Wakati Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS) kikisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar tarehe ya mwisho ya Dk Shein kuingia ofisini ni leo Novemba 2, polisi kwa upande wao wanasema Rais huyo anatakiwa kushika madaraka hayo hadi pale rais mpya atakapoapishwa.
Rais wa ZLS, Awadh Ali Said alisema mwishoni mwa wiki kuwa moja ya athari za tamko la Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi wa Zanzibar ni kusababisha mgogoro wa kikatiba hasa katika muda wa rais kushika madaraka.
Said alisema Ibara ya 28 (2) ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 inaeleza kuwa Rais ataacha madaraka yake baada ya kumalizika miaka mitano kuanzia tarehe alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.
Alisema tafsiri yake ni kuwa tangu Dk Shein alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa rais Novemba 3, 2010 atakuwa ametimiza miaka mitano Novemba 2, 2015.
“Hivyo akiendelea kushikilia madaraka ya urais zaidi ya tarehe hiyo itakuwa kinyume na Katiba ya nchi,” alisema.
Kutokana na madai hayo, Jeshi la Polisi Zanzibar limewatahadharisha wananchi kutojihusisha na vitendo vya fujo kwa madai kwamba kuanzia leo hakutakuwa na Serikali.
Walichosema ZLS
Kwa mujibu wa Rais wa ZLS, maudhui ya Ibara 28 (1) hiyo ni kumpa uwezo wa kikatiba Rais kuendelea ili kutoa nafasi ya maandalizi ya kula kiapo kwa Rais anayefuata tu na si kuendelea kukaa madarakani bila ya kufanyika kwa uchaguzi au kwa sababu ya Uchaguzi kufutwa.
Hata hivyo Said alisema nchi kuendeshwa muda mrefu bila ya Baraza la Wawakilishi (MBW) kama mazingira yaliyopo yanavyoonyesha ni tatizo.
Alisema Katiba ya Zanzibar imeruhusu hali ya kuendesha nchi bila ya BLW kwa muda usiozidi siku tisini (90) tu kuanzia siku Baraza lilipovunjwa.
“Kwa mazingira tuliyonayo, siku tisini (90) zinazokubalika kikatiba zinaishia Novemba 12, 2015 kwa kuwa BLW lilivunjwa Agosti 13, 2015,” alisema.
Rais huyo wa TLS alionyesha pia hatari ya kuwa na rais ambaye yuko juu ya Sheria na Katiba, akibainisha Ibara ya 37 ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 inayoipa Mamlaka Baraza la Wawakilishi kuondoa kinga ya Rais kutoshtakiwa anapokuwa madarakani kama inavyotolewa na Ibara ya 36 ya Katiba.
Alisema katika mazingira yaliyopo hivi sasa ambapo ifikapo tarehe 12 Novemba, 2015, Baraza la Wawakilishi halitakuwapo na haliwezi kuitishwa kikatiba, ni wazi kuwa ikiwa Rais atafanya matendo yoyote yenye kuvunja katiba ya nchi na kukiuka kiapo chake, hakutakuwa na mamlaka nyingine yoyote yenye uwezo wa kuhoji matendo ya Rais.
Alidai hii inatoa fursa na inatengeneza hatari ya kuwa na Serikali inayoongozwa na ‘dikteta’.
Kauli ya Polisi
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alisema jana kuwa kutokana na taarifa hizo za wanasiasa na watu wengine, huenda wananchi watakuwa huru kufanya watakavyo na hivyo kuvunja sheria.
“Tunawaomba wananchi kuacha ushabiki na jazba ili kuwaepusha na gharama za matatizo, wao wenyewe na familia zao. Waswahili wanasema ‘vyako ni vyako, likikupata ni la kwako na kila mchumia janga hula na mwanawe’,’’ alisema Kamishna Makame.
Makame alisema ni vyema kipindi hiki kuhubiri amani na kuwa na subira kuiachia ZEC ambayo ndiyo yenye dhamana na mamlaka ya kutangaza tarehe ya kurejewa kwa uchaguzi na si mtu mwingine.
Kamishna Makame alinukuu kifungu cha 28 (1) cha Katiba ambacho pia wanasheria wa ZLS walikitoa na kumwomba Rais wa Zanzibar kuchukua tahadhari ili asiwe wa kwanza kuvunja Katiba ya Zanzibar kwa kuvuka terehe ya mwisho kuwapo madarakani.
Kifungu cha 28 (1) cha Katiba kinasema, “Kufuatana na Katiba hii mtu ataendelea kuwa Rais mpaka (a) Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais, au (b)afariki wakati akiwa Rais, au (c) hapo atakapojiuzulu; au (d) iwapo amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ; au (e) kwa sababu yoyote nyingine ameacha kuwa kiongozi kwa mujibu wa vifungu vingine vya katiba hii.
“Ikumbukwe kuwa kutokuwapo Rais wa nchi kama inavyodaiwa, haimaanishi sheria hazipo na watu wafanye watakavyo. Kuna makosa ukiyafanya moja kwa moja sheria itachukua mkondo wake ikiwamo kufanya kitendo cha uvunjifu wa amani, kufanya maandamano au mikusanyiko ya watu isiyo halali,” alisema kamishna huyo.
Lipumba: Ni jukumu la JK
Sakata hilo la Zanzibar kwa mara ya pili lilimwibua mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akimtaka Rais Jakaya Kikwete kumaliza tatizo la Zanzibar kwa kuiamuru ZEC kumtangaza mshindi wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 ili kuliepusha Taifa lisiingie kwenye machafuko.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lipumba alisema ni muhimu Kikwete akahakikisha anatekeleza hilo kabla ya kumaliza muda wake, badala ya kumwongezea matatizo na mzigo rais mpya, Dk John Magufuli anayetarajiwa kuapishwa Novemba 5.
“Alhamisi ijayo Dk John Magufuli ataapishwa kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania, Kikwete usimwongezee Magufuli matatizo, yaliyopo yanamtosha,” alisema Lipumba ambaye wiki iliyopita akizungumzia pia mgogoro huo akiitaka ZEC imtangaze mshindi.
Lipumba aliyepokewa na wafuasi zaidi ya 100 kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni , Dar es Salaam, alisema amelazimika kutoa ushauri huo baada ya kuona hatari iliyo mbele, iwapo wananchi wa Zanzibar watanyang’anywa haki yao.
“Vigogo wa Tanzania na Zanzibar wasisubiri hadi maafa yatokee ndipo waanze kuchukua hatua, watumie muda huu kuyazuia,” alisema na kuonya:
“Nayakumbuka mauaji ya wafuasi wa CUF yaliyotokea mwaka 2001 na wengine kukimbilia uhamishoni Shimoni nchini Kenya, nimeona kukaa kimya kutaleta madhara katika nchi hii,” alisema.
Mmoja wa wanachama wa chama hicho, tawi la Buguruni, Ashura Mohammed alisema ni muhimu Wazanzibari wapewe haki yao kwa matokeo ya uchaguzi walioufanya kutangazwa.
ADC : Jecha, ZEC wamekosa sifa
Wakati huohuo, Mwenyekiti wa chama cha ADC, Said Miraaj Abdulla amesema ZEC chini ya Jecha Salim Jecha haiwezi kusimamia tena uchaguzi wa Zanzibar baada ya siku 90 kwa sababu ina mapungufu mengi kama ilivyoyaainisha yenyewe.
Abdulla alisema sababu zilizotolewa na Jecha kufuta matokeo hazina mashiko, zimelenga kuficha ukweli na kutetea maslahi ya upande mmoja. Alisema chama chake kitasimamia haki na ukweli kuhakikisha kwamba matakwa ya wananchi yanasikilizwa.
“Kwanini Jecha aje leo kutueleza kuwa tume yake iliingiliwa na wanasiasa? Siku zote alikuwa wapi na alichukua hatua gani katika kuhakikisha tume yake inakuwa huru,” alihoji mwenyekiti huyo na kusisitiza kuwa kuna ajenda inafichwa na Jecha.
Mwenyekiti huyo aliendelea kusema, Jecha alisisitiza katika matamshi kwamba wajumbe wa ZEC walikuwa wamegawanyika kwa misingi ya vyama vyao lakini hakueleza ni kwa namna gani mgogoro wa wajumbe hao umeathiri kura zilizopigwa.
Aliwataka viongozi kuwa makini na matamshi yao ili yasije kusababisha migogoro na kuvunja amani ya nchi na vyama vyote kuwa na sauti moja ili viweze kutetea haki za wananchi wa Zanzibar ambao wamechagua viongozi wao kwa misingi ya kidemokrasia.
“Viongozi wa CUF na CCM waache kuangalia maslahi ya vyama vyao bali waangalie maslahi mapana ya umma. Chama changu kiko tayari kushirikiana na chama chochote katika kuhakikisha kwamba suluhu ya mgogoro huo inapatikana,” alisema.
Imeandikwa na Salma Said, Raymond Kaminyoge na Peter Elias Mwananchi
utawala wa kimabavu usiozingatia sheria,mwongozo wala kanuni za kidemokrasia umesimikwa zanzibar leo jumatatu tarehe 2 novemba 2015.utawala huo wa kiimla uunaongozwa na dr.ally momamed shein mtawala aliyemaliza muda wake akitokea chama cha mapinduzi;ccm] ambacho kilishindwa vibaya uchaguzi wa rais wa zanzibar jumapili iliyopita tarehe 25 octoba 2015.mshindi halali wa kiti cha urais zanzibar, seif sharrif hamad anatambuliwa na jumuia ya kimataifa ikiwemo marekani,uingereza,jumuia ya nchi za ulaya na mataifa kadhaa ya ulimwengu waliotuma wawakilishi wao kusimamia misingi ya demokrasi haki na usawa wakati wa zoezi zima la uchaguzi.
ReplyDeleteMaalim Seif ni mshindi halali wa kiti cha uraisi kwa mujibu wa taarifa ya tume ipi?
DeleteAcha upotoshaji na uchochezi.Na kama una imani kuwa Maalim Seif atasimikwa uraisi na jumuia za kimataifa basi ndugu yangu utasubiri sana.
ni kikwete aliyeusimika.tunaiomba jumuia ya kimataifa iiadhibu serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania juu ya uhusika wa rais anayemaliza muda wake kuitolea amri ZEC kuufuta uchaguzi mkuu wa zanzibar ambao ulifanyika na kukamilika salama.tufungiwe misaada yote,viwekwe vikwazo vya kusafiri kwa rais na mawaziri wake,budget support ifutwe,agoa isimamishwe,millenium a/c izuiwe na kufutwa kabisa.JUMUIA YA KIMATAIFA KAMWE HAIWALEI MADIKTETA.wacha mkate uuzwe laki moja maduka teule.
ReplyDeleteHata Yeriko Nyerere alitoa uzushi na uchochezi kama wako,hakikisha una ushahidi wa unayoyaandika..
Deleteunatoa vitisho kwa wapiga kura wa zanzibar tulioamua kupitia sanduku la kura.unasema unataka ushahidi wa ushindi seif sharrif hamad?shahidi mkuu ni jecha salum jecha.hebu jitambulishe hadharani ukione cha moto.
ReplyDeleteKama mwanasheria anatafisiri sheria kwa kusoma kifungu kimoja kama layman, basi hakuna haja ya mtu kutumia miaka mingi akisoma sheria! Tafisiri ya aina hiyo hutoka kwa viumbe wenye uchu wa madaraka kama Seif. Ndiyo maana alidiriki hata kujitangaza mshindi wa uchaguzi huku akijua jukumu hilo kisheria ni la ZEC pekee yake!
ReplyDeleteKiufundi, katika mazingira kama haya, dhamana ya urais inaendelea kubaki kwa aliyekula kiapo cha uaminifu kwa nchi na katiba yake hadi hapo atakapoapishwa mtu mwingine kushika dhamana hiyo. Hakuwezi kuwa na vacuum katika dola hata kwa siku moja!
NCHI KUWA VACUUM KIUTAWALA?UNASEMA NINI WEWE?KWA NINI JAJI MKUU ASIAPISHWE KUKAIMU?HALAFU HAINA HAJA YA UCHELWESHAJI WA HILA KAMA HUU TUNAOUSHUHUDIA,UNASEMA NGOJA NIWASILIANE,UWASILIANE NA NANI JIPE MOYO ULIKWISHAANGUKA,RUDI URAIANI.NI KWELI INAUMA SANA,LAKINI HAKUNA JINSI,ONDOKA!
ReplyDeleteHivi wewe siku zote ni mtu wa pumba tu?
Delete