Tingatinga likibomoa moja ya nyumba iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara eneo la Mwenge barabara ya TRA leo asubuhi. Wakazi waishio Mwenge waliotakiwa
kuondoka na Serikali maeneo hayo kwa kuwa sio sehemu rasmi na nyumba zao kuwa
zimewekewa alama ya mkasi wabomolewa nyumba zao,jijini Dar es
Salaam. Zoezi hili linaonekana ni muendelezo wa Bomoa bomoa maeneo ambayo
yashaakatazwa na ikikumbukwa ni siku chache tu wakazi waliokuwa wanaishi eneo
la kidongo chekundu kurasini nao kukumbwa na kadia hii.Picha na Geofrey Adroph
wa Pamoja Blog
Tingatinga likiwa limemaliza kubomoa moja ya nyumna eneo hili la mwenge jijini Dar
Baadhi ya vyombo pamoja na vifaa mbalimbali vilivyookolewa katika eneo la ubomoaji uliofanyika leo Mwenge eneo la Barabara ya TRA leo asubuhi. Ubomoaji huu umeanza saa kumi za alfajiri na kumalizika saa tatu za asubuhi.
wananchi wakishuhudia ubomoaji huo ambapo ulinzi uliimarishwa vizuri.
Hakika ulinzi ulikuwa ni wakutosha wakati wa zoezi la bomoa bomoa lililofanyika leo Eneo la Mwenge barabara ya kwenda TRA
Hali halisi baada ya tingatinga kubomoa majengo yaliyojengwa kwenye hifadhi ya Barabra
Wafanyabiashara wakiokoa baadhi ya mali zao kutoka kwenye vifusi vya udongo na mabati baada ya kubomolewa maeneo yao ya biashara leo asubuhi
Tingatinga likiendelea na kazi
No comments:
Post a Comment