Wednesday, November 4, 2015

WANANCHI WATAKIWA KULINDA AMANI YA NCHI - CP CHAGONJA



Na Chalila Kibuda
JESHI la Polisi limewataka wananchi kuendelea na utulivu kama walivyoonyesha wakati wa upigaji kura na hatimaye kupatikana katika siku ya uampishwaji wa Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja amesema kuwa jeshi la polisi limeridhishwa na utulivu uliokuwepo wakati wa upigaji kura, na utulivu huo umeweza kufanya uchaguzi kwenda salama na hatimaye kukaweza kupatikana mshindi.


Amesema katika suala la Zanzibar liko katika mazungumzo na viongozi wanafanya kazi yao hivyo maandamano hayana nafasi kutokana na taratibu wanazozitumia.


Chagonja amesema watu waliokamatwa katika vurugu za uchaguzi wamefikishwa mahakamani na huku wengine wakiendelea na uchunguzi.


Amesema hali ya amani ipo na wananchi wametakiwa kulinda hali hiyo na ikitokea mtu analeta uchochezi walipoti kwa vyombo vya usalama ili hatua zichukuliwe.
Chagonja ametaka baadhi ya taarifa katika mitandao ya jamii kuupuzwa ,kwani zinatoa taharuki kwa wananchi na zinapotosha.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake