ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 14, 2016

BEKA IBROZAMA - YOU AND I - OFFICIAL VIDEO


Happy Valentine’s Day.  Siku ya wapendanao hainogi bila kuwa na maua makundu na muziki mzuri wenye ujumbe mahsusi. 

Wakati ukiitumia siku ya leo kuimarisha upendo wako na yule umpendaye, Beka Ibrozama amekusaidia kwa kukupa wimbo huu maalum kwa siku ya leo. 

Wimbo unaitwa ‘You and I’ ambamo humo ameimba kwa lugha nne tofauti – Kihindi, Kiingereza, Kiswahili na Kilingala. 



“Kama kawaida mimi hupenda kuonesha utofauti kwenye nyimbo zangu. Awamu hii nimeamua si kuimba tu lugha nne bali pia kutengeneza wimbo wenye mahadhi tofauti,” anasema Beka.

“Ukisikiliza utasikia R&B, Bongo Flava na Nachi lakini pia mwishoni wimbo nimeubadilisha kabisa na kuwa na majadhi ya Lingala, naamini mtafurahi,” ameongeza.

“Nawatakiwa happy Valentine’s Day na nitafurahi kama ukitumia wimbo huu kupeleka ujumbe kwa umpendaye.”

Wimbo huu umetayarishwa na producer mwenye ubunifu na uwezo wa hali ya juu katika kutengeneza nyimbo za mahadhi mbalimbali, Shantee aka Mkongo.

No comments: