Bryan Mwombeki akiwa na kombe lake baada ya mchuwano mkali na Dada yake KageBriana.
Watoto wenye asili ya Kitanzania mtu na dada yake waling'ara kwenye michuano ya tennis kombe la Valentines iliyofanyikia Washington, DC
Patashika lilihibuka pale ambapo mtu na dada yake walichuana vikali katika unyakuzi wa kombe la valentines Tennis watoto lililofanyika katika viwanja vya ndani vya SETLC mjini Washington, DC.Mpambano huo ulifanyika siku ya ijumaa jioni,Februari 12 baada ya Bryan mwombeki kumshinda mpinzani wake Jewel Peterson Bao 6-0 katika mechi ya kwanza. Naye Briana Kagemuro alimshinda mpinzani wake Jacob Poole mabao 6-1.
Mchezo wa mwisho kumtafuta mshindi ulinoga baada ya mpambano kuwa wa mtu na dada yake. Bryan Mwombeki aliibuka mshindi kwa kushinda bao 6-4 dhidi ya Dada yake Briana kagemuro. Kwa matokea hayo Bryan Mwombeki aliibuka mshindi wa kwanza na Dada yake Kage Briana kubeba ushindi wa pili.
Briana akiwa na kombe lake la mshindi wa Pili Tennis watoto,Washington, DC
Mama ya watoto Bryan na Briana Bi. Bernadeta kaiza akiwapongeza watoto wake.
No comments:
Post a Comment