Utendaji wa Rais John Magufuli baada ya siku 100 tangu alipoanza rasmi kazi kama kiongozi wa ngazi ya juu zaidi nchini, umezua mijadala mingi huku asilimia kubwa wakimpongeza kwa kazi nzuri lakini wengine wamesimama na yao.
Muendelezo wa kuchukua maoni ya wanasiasa wakongwe, wadau wa maendeleo na wananchi wa kawaida umegonga mwamba kwa mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na kupelekea kuivunja ahadi yake aliyoitoa awali kuwa angempima Rais Magufuli baada ya siku 100.
Kingunge ambaye alitangaza kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuiweka kando kadi yake namba 8 baada ya kukitumikia chama hicho kwa zaidi ya miaka 60, na kumpigia debe Edward Lowassa (Chadema), amekataa kuikamilisha ahadi yake ya kuuzungumzia utendaji wa Magufuli huku akieleza kuwa hakuna mtu wa kumlazimisha kuitimiza ahadi hiyo.
“Hata kama niliahidi kuzungumza baada ya siku 100 lakini hakuna mwenye uwezo wa kunilazimisha kuzungumza,” Kingunge anakaririwa na gazeti la Nipashe. “Sitazungumza, waulizeni wengine watasema lakini mimi naomba mniache,” aliongeza.
Kingunge alitangaza kujieungua CCM kwa madai kuwa chama hicho kimevunja katiba wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wake wa urais na kwamba kimepoteza dira kwa kuacha misingi ya uasisi wake.
CHANZO:: NIPASHE
CHANZO:: NIPASHE
10 comments:
Mwacheni Mzee Kingunge apumzike. Kichwa chake kimechoka. Amefikia kipindi kile ambacho wazee wengi wa rika yake hawawezi kutofautisha ukweli na uongo, jana na leo, usiku na mchana, na kadhalika. Unadhani maoni yake ni muhimu kwa Magufuli? SASA KAZI TUU!
wala hatuna haja tusikie unaongea nini juu ya rais wetu mpendwa MAGUFULI kwani sisis tumeishakubali kazi yake inatosha na wewe KINGUNGE ni binadamu tu kama sisi wengine,kwanza ni aibu zako na wivu kwa rais wetu ndio unaendekeza na ndio ulisababisha wenzako wakose kuongoza nchi,tunaomba ukae pembeni KINGUNGE usije tuletea matatizo kwa raisi wetu.
Kingunge,kachoka mbaya,sana,lakini bado,anajitia bado yumo.akalala tu kilwa,aache,kushanga ,shangaa,kushangaa,mwisho,ni mara moja.
Kingunge has always been a con politician - in and outside of CCM. He continues to be what he has always been; a con man. But he has one reached the end of the road. You can fool some people some of the time but you cannot fool all the people all the time.
Had he had any semblance of principles it should not have been too hard for him to notice the transformation Magufuli is leading in the country. However, as a con man he is too indebted to his handlers, aka Lowassa!
Nani anangoja Kingunge aongee? Lowassa ama mwendawazimu! Hawaoni yanayoendelea nchini?
Yaani kweli mnamshambulia mtu kwa kukaa kimya?? Hiyo ni haki yake ya kidemokrasia.Anayo haki ya kukaa kimya au kuongea.Hata kama wewe ni mshabiki wa Magufuli huwezi kuwalazimisha watu kumshabikia.Kingunge ni mtu mzima na ambaye yuko kwenye siasa tangu nchi inapata uhuru na AMEONA MENGI hivyo ni busara kumpa muda wake na akiwa tayari ataongea.Tusiwe watu wa kufuata HISIA NA MIHEMKO YA HARAKA HARAKA TUIJENGE NCHI YETU KWA HAKI KWA KILA MTU....
Baada ya kuona mengi mazuri ambayo Rais Magufuli anayayoyafanya nchini, Kingunge sasa anaona aibu na kujutia maamuzi yake ya purukushani yaliyomfanya kuhama chama alichokitumikia muda mrefu na kufuata msala upitao. Kwa mantiki hii ni vigumu kwa Kingunge kuongea chochote. Ni vizuri kama ataendelea kukaa kimya angalau alinde salio, kama lipo, la heshima yake yoyote ile ambayo itakuwa bado imebakia katika duru za kisiasa.
eti hapa kazi tu wakati watu hawana kazi.wezi wajanja wachumia tumbo bado wanapeta eti tunatumbua majibu thubutu uwaguse the untouchable. kingunge ndo dume la mbegu kishaona usanii huu ndo maana anakaa kimya.wenye mihemko na mzee maguu ndo utaona wakimshambulia kingunge. maana wameshazoea sanaa za maigizo.
ukifanyakazi lazima uwaonyeshe watu unafanya kazi au kuwalazimisha watu wafanye kazi ili iweje.kuna mwisho wa haya makelele ya slogan hapa kazi tunausubiri hatuna mihemko ya ushabiki maandazi tunatizama mwisho wa movie hii ikoje.
kama kweli magu ana nia njema na nchi hii basi arudishe rasimu ya katiba.waiba kuku wanafungwa miaka 20 mafisadi wanatamba mitaani halafu tunatumbua majibu thubutu.wadanganywe hao hao nyumbu.wasiojua mambo yanavyokwenda katika nchi hii.wanaojua wanapiga kimya kama kingunge alivyofanya.
Miezi iliyopita ni michache kuliko miaka iliyopo mbele.Tusubiri jamani safari ndefu.Hata mimi HAPA KIMYA KWANZA.
Post a Comment