Familia ya PCP (Rtd) Nicas Pius Banzi wa Ukonga Dar es Salaam inayoheshima kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba, mazishi na hatimaye matanga ya mama yetu mpendwa LYDIA JACOB BANZI aliyefariki dunia January 21, 2016 katika hospitali ya Rabininsia na Kuzikwa katika Makaburi ya Pugu Dar es Salaam January 24, 2016.
Kwa vile waliotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi hiki kigumu cha msiba ni wengi na ni vigumu kuwataja kwa majina. Familia, inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za Jumla ikiwa omba kuzipokea shukrani hizo kwa moyo ule ule kama milivyo tuunga mkono.
Hata hivyo tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa madaktari na wauguzi wote wa Muhimbili (MOI) hospitali waliomuhudumia marehemu katika kipindi cha ugonjwa wake na mpaka umauti ulipomkuta. Tunashukuru Uongozi wa Jeshi la Magereza Tanzania, Parokia ya Mtakatifu Agustino Ukonga ikiongozwa na Baba Paroko Steven Nyilawila, Jumuiya ya Mtakatifu Anna, Baba Askofu Antony Banzi wa Jimbo katoliki la Tanga, Viongozi waandamizi na wastaafu wa serikali waliofika kutufariji wakiongozwa na waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda.
Tunawashukuru Sana. Mungu Awabariki.
No comments:
Post a Comment