ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 14, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA MUHIMBILI KUKAGUA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS MAGUFULI


FSA_6533

Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.
FSA_6416 FSA_6443
????????????????????????????????????
FSA_6540
????????????????????????????????????

2 comments:

Anonymous said...

Pamoja kazi nzuri anayofanya JPM,ifike wakati waanze kuweka mifumo (system ) zitakazo simamia shughuli zakiutendaji hata bila ya raisi,waziri mkuu kufumania.
Kilichopo sasa hivi,nikuwa viongozi wetu wengi wamekosa ubunifu,na mindset zao zilidumazwa na mfumo wa boraliende,cannot see right or wrong. .Itakuwa ngumu kwa JPM kupata mafanikio chanya kwakutumia mfumo wa uendeshaji wa bora liende,watafukuzwa wengi lkn kama mfumo ni uleule itakuwa ngumu kufanikiwa.

Unknown said...

Hospitali za Mikoa na Wilaya lazima ziboreshwe kupunguza msongamano Muhimbili