Daraja la Kigamboni limefunguliwa sasa Tanzania ni moja ya nchi yenye madaraja ya kuvutia katika ukanda wa Africa kutokana na muonekano wa taa nyakati za usiku daraja hili lipo kwenye top 3 katika madaraja matatu makubwa yaliyopo Tanzania kwa sasa. Kwanza daraja la Mkapa lilipo barabara ya Kusini na daraja lingine ni lile linalo unganisha Tanzania na Mozambique.
Tukizungumzia Daraja Bora lenye mvuto wa aina yake katika nchi zote za Ukanda wa Afrika Mashariki hutaacha kulitaja Daraja la Kigamboni linalopatikana Dar es Salaam Tanzania pekee lakini kubwa zaidi ndio Daraja pekee linalopita juu ya maji.
Daraja hilo limetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya matumizi ya kamba (Cable) kubeba uzito wa daraja, ambalo linaunganisha jiji la la Dar es Salaam na eneo la Kigamboni na Kurasini.
Pamoja na kujengwa katika ubora wa hali ya juu, daraja hili lina jumla ya njia sita yaani njia tatu kwa kila upande, pamoja na njia mahususi kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli ambayo ina upana wa mita 2 na nusu (2.5 meters) katika kila pande likiwa na uwezo wa kupitisha magari yenye uzito usiozidi tani 30.
Watanzania wanajivunia kuwa na daraja zuri, la pekee Afrika ya Mashariki linalopita baharini lenye kuvutia kutokana na muonekano wake hasa nyakati za usiku.
Hadi kukamilika kwa ujenzi wake Daraja la Kigamboni limegharimu kiasi cha dola milioni 135 sawa na shilingi bilioni 283 likitazamiwa kuzinduliwa rasmi Aprli 19 na Rais Dk. John Magufuli.
Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-
1) Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu miundombinu ya daraja
2) Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
3) Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo hicho.
4) Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
5) Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.
Aidha, Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.
Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.
Tazama picha zinge za Daraja la Kigamboni hapo chini
Jitiririshe hapa chini kwa picha zaidi.

1 comment:
Tatizo si kushangaa, shida ni uchafu na vibaka
Post a Comment