Saturday, April 23, 2016

IDADI YA WATUMISHI HEWA MKOANI IRINGA YAONGEZEKA

 Mkuu  wa  mkoa wa  Iringa Mhe. Amina  Masenza  akizungumza na  wanahabari  mjini Iringa leo 

Ndugu Waandishi wa Habari,
Hadi kufikia tarehe 18/04/2016 Mkoa wa Iringa umefanya zoezi la uhakiki wa watumishi kwa awamu mbili awamu ya kwanza, uhakiki ulifanyika kuanzia tarehe 16/03/2016 na kukamilika tarehe 26/03/2016 ambapo jumla ya watumishi 15 walibainika kuwa ni watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa ambao waliisababishia Serikali hasara ya Shilingi 81,921,725.08. 
Katika uhakiki wa awali Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo haikuwahakiki watumishi 159 kutokana na kuwa masomoni. Halmashauri hiyo imekamilisha uhakiki huo ambapo imebainika watumishi wawili (2) ni watumishi hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuhakikisha Mkoa unaondokana kabisa na tatizo la watumishi hewa, niliwaelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya zoezi hilo awamu ya pili. 
 Nimepokea taarifa kutoka kwa Wakuu wa Wilaya inayoonesha kuwapo kwa watumishi hewa kumi na mbili (12) hadi kufikia tarehe 18/04/2016. Watumishi hao wameisababishia Serikali hasara ya shilingi 155,205,681/=

Watumishi hao wapo katika mchanganuo ufuatao:
NA
HALMASHAURI
WATUMISHI HEWA WALIOBAINISHWA AWALI
WATUMISHI HEWA WALIOBAINISHWA SASA
JUMLA
1
H/W Iringa
2
7
9
2
H/W Kilolo
6
2
8
3
M/Mji Mafinga
3
0
3
4
H/W Mufindi
4
0
4
5
H/Manispaa
0
3
3
JUMLA
15
12
27
 Uhakiki uliofanywa na Mkuu wa Wilaya katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umebainisha kuwapo kwa watumishi tisa (9) ambao ni watoro na mtumishi mmoja ambaye aliomba likizo bila malipo na kwenda kufundisha mahala pengine lakini akaendelea kulipwa mpaka kufikisha  kiasi cha Tsh. 25, 831,000/= lakini baada ya kufanya ufuatiliaji amerejesha kiasi cha Tsh. 18,604,679/= Mtumishu huyu ni mwalimu anaitwa Dinner J. Kissamo alikuwa mwalimu Manispaa ya Iringa.   
Aidha, Uhakiki pia ilibaini mwalimu mmoja (Ifunda) alikuwa na Check Na. 2 na zote alikuwa analipwa na halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika. 
Mtumishi Mwingine ni Khalid M. Meza Afisa kilimo Kilolo ni  mtoro wa muda mrefu mkurugenzi tayari ameshamfungulia mashtaka. Hii ni mifano tu ya watumishi hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuendelea kujiridhisha  na kuondolewa kabisa watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa, nimechukua hatua zifuatazo;


1.    Nimewaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa, zoezi la uhakiki watumishi linakuwa endelevu na hatua zinachukuliwa ili kuwaondoa watumishi hewa wote           

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake