Friday, April 22, 2016

Mama mtoto wa Nay wa Mitego kafungwa miaka miwili Jela



Ni stori iliyoanza kuchukua headlines April 21, 2016 Ikiwa bado tunasubiria taarifa kamili kutoka Mahakamani, sasa Ayo TV ilimpata staa Nay wa Mitego kuthitibisha taarifa hizo za mzazi mwenza, Siwema kufungwa miaka miwili Jela.
Ni stori iliyoanza kuchukua headlines April 21, 2016 Ikiwa bado tunasubiria taarifa kamili kutoka Mahakamani, sasa Ayo TV ilimpata staa Nay wa Mitego kuthitibisha taarifa hizo za mzazi mwenza, Siwema kufungwa miaka miwili Jela.

Akizungumza staa huyo na ripota wa Ayo TV alisema…>>>’Taarifa nimezipokea ni kweli Mzazi mwenzangu amefungwa na ninakumbuka nilipoamka tu nikakutana na missed calls za ndugu zake kadhaa ambao wananifahamu nikahisi kuna kitu maana sio kawaida watu kunipigia mara kwa mara, kumpigia akaniambia Siwema amehukumiwa miaka miwili Jela sikuamini ikanibidi nimpigie tena ndugu wa karibu naye akanithitibishia hivyo‘ – Nay wa Mitego

‘Kosa unajua mimi nilishasahau kwamba kitu chochote kichotokea kipindi cha nyuma kwasababu ni muda kidogo na pia sikuwa naye kwenye mawasiliano ila niliachoambiwa kuwa amehukumiwa miaka miwili kutoka na kosa lake, nimejikuta nimekuwa mnyonge nimeingia imani kusikia habari hiyo’ – Nay wa Mitego

Unaweza ukabonyeza play kutazama interview ya Nay wa Mitego akizungumza kuhusu kufungwa kwa Mzazi mwenza miaka miwili Jela

1 comment:

  1. Vijana wa kibongo bwana... hukumu imetolewa mahakani ambapo kila kitu kilikuwa wazi sasa wewe unashundwa nini kuzungumzia tatizo lilopelekea huyo mdada kufungwa. Badala ya kujibu swali wewe unaleta story tuuu . Jifunze namna ya kujibu maswali.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake