Jioni ya jana Jumamosi (16/04) Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston na miji mingine ya karibu ilifanya Ibada Takatifu katika kanisa la Umoja kumuaga mpendwa wao Henry Kiherile aliyefariki wiki moja na nusu iliyopita baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Ibada hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa na huzuni kubwa juu ya kifo hicho kilichogusa mioyo ya watu wengi. Mwili wa marehemu Henry unatarajiwa kusafirishwa jioni ya leo kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 22/04/2016. Pata picha za Misa hiyo hapa chini.
Marehemu Henry Kiherile enzi za uhai wake |
Gari lililobeba mwili wa Henry likiingia kanisani |
Wachungaji wakiwa nje ya kanisa kabla ya ibada |
Jeneza lililobeba mwili wa Henry likiingizwa kanisani |
Dada Lulu ( mdogo wa Marehemu Henry ) akimuaga kwa uchungu kaka yake |
Mr. & Mrs. Tenende ( Baba na Mama mkubwa wa marehemu ) wakiwa kanisani |
Waombolezaji wakilia kwa uchungu |
Rafiki wa Henry kutoka Cameroon |
Waombolezaji |
5 comments:
Henry upumzike kwa Amani .poleni wakina makinda.Huyo mama ake mkubwa ni mdogo wa Annie makinda .Huyu henry Annie makinda mama Yake mlezi.
inasikitisha sana jamani na poleni sana sana,sijui mama yake na ndugu zake Tz watampokeje Mwenyezi M ungu wape nguvu.
Namuona Andrew Sanga akiwa miongoni mwa waagaji bila kujua usiku ilikua ni zamu yake. Mwenyezi Mungu amsimamie aweze kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida
Gone too soon! May he rest in peace.
What is going on in Texas??
Rip.
Post a Comment