ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 18, 2016

RAIS MAGUFULI AMTEUA CHIKAWE KUWA BALOZI JAPAN

Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe. Picha kutoka Maktaba

 Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa balozi wa Tanzania nchini Japan.
Taarifa iliyotolewa leo 18 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Chikawe umeanza Aprili 13, 2016.
Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo Februari 15, 2016.
Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

4 comments:

Anonymous said...

I thought we rejected him in the last elections, but he is good enough to represent us in the next 5 years, Bongoland politics.
I thought he retired sometime ago last year.

Anonymous said...

Zilipendwa??

Anonymous said...

Atarudi akiwa 85, where are all the young people at Foreign Affairs

Anonymous said...

when will then retired remain retired so we young people can get opportunities.....