RATIBA YA SHUGHULI ZA MSIBA WA ANDREW "404"SANGA.
Hapa
Chini ni ratiba ya shughuli zinazoambatana na msiba, taarifa zilizomo ni kutoka Kamati zinazohusika na majukumu husika.
1)HARAMBEE (Kesho 04/23/16)
Tutakuwa na harambee kuchangisha fedha za kusafirisha mwili na Gharama zinginezo hapo LEO Jumamosi April 23, 2016 kwenye ukumbi huu hapa chini kuanzia
saa tisa Alasiri (1500 Masaa ya Kijeshi)
11916 Bissonett Suite #170
Houston, TX 77099
2)HUDUMA ZA KIROHO NA KUAGA MWILI (04/30/16)
Kutakuwa na Huduma za Kiroho na kuuaga mwili wa Marehemu Jumamosi IJAYO,tarehe 04/30/16 kuanzia SAA SABA MCHANA (1300 Masaa ya Kijeshi) kwenye Kanisa hili hapa chini:
CHIRST THE SERVANT LUTHERAN
CHURCH
Anwani : 2400 S. Wilcrest Dr
Houston, TX 77042
Wanajumuia tunasisitizwa kujali
Muda uliotajwa kwani ratiba itazingatiwa ili kuweza kupisha huduma zingine za Kiroho ziendelee Kanisani hapo.
***SISITIZO: Hapa ndipo patakuwa mahali pekee pa kuweza kuaga mwili wa Marehemu na kutoa heshima za mwisho.
***USHAURI: Tafadhali kwa tunaojua hatotoweza kuhimili hisia zetu tunao uamuzi wa kutoshiriki tendo hili. Tuamue kwa busara zetu kadri dhamira zetu zitakavyotutuma.
3)KUSHEREHEKEA MAISHA YA ANDREW: (30/04/16)
Wanajumuia wameona ni vyema kusherehekea maisha ya Andrew kwa kukutana na kujifariji pamoja kuanzia saa kumi na mbili jioni
Tutakutana Jumamosi baada ya Kuuaga Mwili kanisani kwenye ukumbi wa Harambee kwa Misa Maalumu itakayofuatiwa na chakula cha pamoja tukisherehekea maisha yetu na Andrew kwa pamoja.
Sienna Hall
11916 Bissonett Suite #170
Houston, TX 77099.
Kny,Kamati ya Mazishi
Saidi Nusura, Katibu
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake