Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.
Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi.
Papa Wemba akiwa jukwaani kwa mara ya mwisho jijini Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake