Friday, April 22, 2016
Tay Grin ft 2 Face Idibia - Chipapapa
Malawi na Nigeria zimekutana kwenye collabo moja ya nguvu. Supastaa wa rap kutoka Malawi, Tay Grin ameachia single mpya aliyoipa jina, Chipapapa na kumshirikisha nguli wa muziki wa Nigeria, 2 Face Idibia aka 2 Baba.
Ngoma hii kali na ya kuchezeka, imetokana na urafiki wa muda mrefu kati ya wasanii hawa.
“Nimemfahamu 2 Baba kwa miaka mingi na tumekuwa tukiongea siku zote kuhusu kolabo. Ni msanii mwenye kipaji kikubwa na kufanya kazi naye ni furaha kubwa kwangu,” anasema Tay.
Akiutambulisha Chipapapa kwa wapenzi wa muziki Afrika Mashariki, Tay ametoa ujumbe huu kwao: Nikijitambulisha tena kwa Afrika Mashariki, ningependa kuwashukuru mashabiki wangu wa kitambo kwa kuniunga mkono pamoja na muziki wangu. Kwa mashabiki wangu wapya, salamu za pekee kutoka Malawi kwenu nyote. Nina hamu kubwa ya kuja kwenu na kuwaburudisha.”
Video ya Chipapapa ilifanyika Afrika Kusini kwenye mji wa machimbo ya madini wa Nigel na kuongozwa na Bruce Patterson. Ni video inayoonesha uzuri wa Afrika kwa kutumia uchezaji, rangi na watu wazuri waliovaa nguo mbalimbali za Kiafrika.
Tay Grin amechukua mchezo wa kizamani wa Kimalawi na kuuweka katika wimbo. Chipapapa ni mchezo ambao wengi waliufarahia enzi wakiwa watoto.
“Ni mchezo unaotukumbusha wengi wetu katika muda fulani wa ujana wetu,” amesema Tay na kuongeza, “2 Baba kisha alilielewa wazo na kwa haraka akaongeza michezo mingine waliyonayo Nigeria.”
Tay Grin ana orodha kubwa ya kolabo alizowahi kufanya ukiwemo wimbo ‘Nyau’ aliomshirikisha mshindi wa tuzo za MTV, Nameless wa Kenya.
Muziki wa Grin unawalenga vijana na kuwataka wajivunie nchi zao na utamaduni wao. Kuwajibika, kutumia vipawa walivyopewa na Mungu na kutafuta thamani katika kuchangia mustakabali mzuri. Pia kusisitiza hitaji la kuondoa mambo hasi na kutojikatia tamaa.
Akianza kufanya rap tangu akiwa mdogo, Tay alivutiwa na wasanii wakongwe kama Jay Z, KRS 1, B.I.G na Tupac. Ili kupata aina yake tofauti ya rap, Tay aliangalia ladha za Kiafrika na utamaduni wa Malawi kumsaidia kutengeneza mtindo wake wa pekee.
Tay amewahi kutumbuiza kwenye shindano la Big Brother Africa (2007/2008)
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake