Saturday, April 23, 2016

TFDA YAKAMATA SHEHENA KUBWA YA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti B. Sillo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya vipodozi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti B. Sillo akitowa maelekezo kwa maofisa wa (TFDA.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Jeshi la Polisi, imefanyaukaguzi maalum na kufanikiwa kukamata shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Serikali katika baadhi ya majengo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na thamani yake haijajulikana mara moja haditathmini ikakapokamilika.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti B. Sillo ambaye alikuwa nimiongoni mwa washiriki wa zoezi hilo kwa masikitiko makubwa, alisema “ Kiasi cha vipodozi hivihatarishi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, ni kikubwakatika historia ya ukaguzi hapa nchini na wafanyabiashara wote wanaohusika na biashara hii haramu ni lazima wachukuliwe hatua stahiki za kisheria”.

Mkurugenzi Mkuu huyo, aliendelea kusema kwamba kwa vile vipodozi hivi huingizwa kwa njia yamagendo, ukaguzi huo ni endelevu na wahusika hawataweza kukwepa mkono mrefu wa Serikali mahalipopote na wakati wowote.

Alitoa rai kwa wafanyabiashara kuacha mara moja kuvunja Sheria za nchi na wasalimishe kwa hiyari yao vipodozi vyote vilivyopigwa marufuku TFFDA badala ya kusubiri Taasisi hiyo iwafuate.Katika hatuanyingine, Mkurugenzi Mkuu huyo aliwaasa wananchi kufanya maamuzi sahihi ya kutumia vipodozisalama vilivyosajiliwa na Mamlaka na kuachana na vile vilivyopigwa marufuku ili kulinda afya zao.Zoezihili limefanyika kuanzia tarehe 21/4/2016 na haikuelezwa mara moja kwamba litaisha lini.
Mafundi wa (TFDA) wakiendelea na kazi.
Afisa wa (TFDA) akiwa amebeba kiroba chenye vipodozi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa (TFDA) wakipakia kwenye gari vipodozi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake