Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza. Mafunzo hayo yameanza leo na yanatarajia kufikia tamati kesho Mei 07,2016.
Na:BMG
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba, amewataka watumishi wa Mahama Mkoani
Mwanza kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na kwa wakati.
Mhe.Makaramba ameyasema hayo hii leo Jijini
Mwanza, wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayoendeshwa na
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa Watumishi
wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza.
Amesema Mafunzo hayo yamekuja kwa
wakati ikizingatiwa kwamba Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na
maboresho ya Utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kwamba inatoa huduma
iliyo bora kwa wananchi.
Mwenyekiti wa taasisi ya MISA tawi la
Tanzania, Simon Berege, amesema mafunzo hayo yanaendeshwa katika Kanda zote za
Mahakama nchini, baada ya utafiti uliofanyika mwaka 2014 kuonyesha kwamba kuna ugumu
katika upatikanaji wa habari za mahakama kwa umma hata kama habari hizo siyo za
siri.
“Tunaipongeza Mahakama kwa hatua hii
ya kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wake na kutoa taarifa muhimu kwa
wananchi maana mihimili mingine imekuwa ikiminya upatikanaji wa taarifa zake
hata kama taarifa hizo siyo za siri”. Amesema Berege.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo
hayo wamesema wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwemo kuongeza ujuzi zaidi wa
namna ya kuwahudumia wateja (Wananchi) ili kuwafanya watambue kwamba Mahakama nchini
zinatenda haki.
Mafunzo hayo ambayo yanafadhiriwa na
Shirika la Misaada la Ujerumani FES, yamefanyika Mkoani Mwanza baada ya mafunzo
kama hayo yaliyofanyika katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Tabora kuonyesha
yameongeza ufanisi na utendaji wa Watumishi wa Mahakama katika kuwahudumia
wananchi hususani katika utoaji wa taarifa kwa umma ambapo yanawajumuisha
Mahakimu, Watunza Kumbukumbu pamoja na Maafisa Utumishi wa Mahakama.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege, akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege, akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege (Kulia), akifurahia jambo wakati wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza. Kushoto ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Wakili na Mwanahabari James Marenga
Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza katika Mafunzo hayo
Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza katika Mafunzo hayo
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza, wakifurahia hotuba ya mgeni rasmi, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza

Mgeni Rasmi, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramaba (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Mgeni Rasmi, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramaba (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
No comments:
Post a Comment