Unadhani kuwa unajua kila kitu kuhusu mume wa
maisha yako? Mahusiano mengi hukoma kwa sababu ya masuala ya mawasiliano, uongo
au shakhsia zisizoendana. Mengine hufikia kikomo kwa sababu wanandoa
hawakuchukua muda kujuana.
Famasia
yako ya Ndoa Maridhawa imekuletea mambo 10 ambayo unatakiwa kuyajua kuhusu
mwanaume wa maisha yako kabla hujachukua hatua zaidi. Iwapo unayajua baadhi,
basi endelea kufuatilia zaidi na zaidi:
1.
MALENGO YA KWELI YA KAZI YAKE
Huwenda
unaijua kazi yake… lakini unajua kuhusu kazi ya ndoto yake? Unajuaje iwapo
atabadili kazi yake baada ya miaka 5? Tambua mapema iwapo mumeo anataka kuwa
meneja, kibarua au mkurugenzi wa kampuni au shirika. Anaweza akawa na wazo la
kumiliki biashara zake mwenyewe.
2.
RADIAMALI YAKE (reaction):
Mzee
wangu mmoja aliwahi kuniambia: “Unaweza kujua kuhusu mtu fulani kwa kutazama
namna anavyoshughulikia mambo”. Kauli hii inatufundisha kujua kuhusu ghadhabu,
hasira na subira ya mtu husika. Hili linaweza kukuonesha namna mtu huyo
alivyo. Kupitia radiamali ya mtu ndipo unapoweza kujua silka yake.
Lizingatie hilo.
3. ENEO
ANALOPENDA ZAIDI DUNIANI
Tambua
eneo analolipenda zaidi katika maisha yake, na ambalo humpatia furaha zaidi.
Wakati fulani utaweza kutumia fursa hiyo kumfanya kuwa mwenye furaha.
Kwa
mfano, mimi ninapenda sana mkoa wa Kigoma… Sio tu kwa sababu ni kwetu, lakini
kwa sababu kuna mambo mengi yenye kuijaza kumbukumbu ya maisha yangu kiasi
kwamba huhisi ombwe nisipoyaona mambo hayo.
4. VIWANGO
VYA MAISHA YAKE
Jitahidi
sana kujua “living standard” yake kabla ya kuingia katika ndoa. Hilo
litakusaidia kujua aina ya mtu unayeingia naye kwenye ndoa na jinsi ya
kuamiliana na hali zenu za kiuchumi.
No comments:
Post a Comment