ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 1, 2016

AHADI YA RAIS MAGUFULI KWA WAFANYABIASHARA WAKUBWA YAANZA KUTIMIA

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda  (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda 2015 (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi wetu
Nia serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuanza kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa nchini ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kusaidia kuinua uchumi wa nchi lakini pia kutoa ajira kwa watanzania katika viwanda vinavyoilikiwa na matajiri hao.

Hilo limenza kuonekana siku moja baada ya Rais Magufuli kuweka wazi nia yake hiyo ambapo Mo Blog ilifanikiwa kupata picha ambayo ilimwonesha Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akizungumza mambo mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Taznzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi mara baada ya kumalizika kwa halfa ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) zilizoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Kutokana na muonekano wa viongozi hao wawili wa serikali na sekta binafsi ni wazi kuwa serikali ya Rais Magufuli imejipanga kushirikiana na wafanyabiashara ili kufanya kazi kwa pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda jambo ambalo litachangia ukuaji wa kasi wa uchumi na upatikanaji wa ajira kwa Watanzania.

No comments: