ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 1, 2016

Hatimaye Siwema wa Nay Atoka Gerezani!

Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Siwema Edson.

Na Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO

HABARI njema! Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kutishia kwa njia ya mtandao, hatimaye ametoka jela.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Nay wa Mitego alisema katika harakati za kushughulikia ili mzazi mwenzake huyo atoke alifanikiwa kupata mawakili wawili ambao mpaka Jumamosi iliyopita walifanikisha zoezi la Siwema kutoka na sasa atatumikia kifungo cha nje.

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake, Siwema Edson

Nay wa Mitego alisema alilazimika kupambana kwa nguvu zote si kwa sababu anataka kuwa naye isipokuwa kama mzazi hakujisikia vizuri kuona mama wa mwanaye yuko jela wakati yeye anao uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya kumsaidia.

“Kulikuwa kuna njia mbili za kufanya, kukata rufaa au kubadilishiwa kifungo, mawakili wangu waliniambia niwaachie wao watamaliza.

“Hivi ninavyoongea na wewe niko mbali na mjini lakini taarifa za Siwema kutoka jela ninazo, kwa hiyo sina maelezo mengine zaidi ya hayo ila namshukuru Mungu kwa kulifanikisha hili,” alisema.

Aprili mwaka huu Siwema alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa kosa la kutoa vitisho kwa kutumia mtandao.

Siwema na Nay walikuwa ni wapenzi wa muda mrefu ambapo walifanikiwa kupata mtoto mmoja lakini akiwa bado mchanga, Nay alimfumania mzazi mwenzake huyo na mwanaume mwingine na hivyo kuvunja uhusiano wao huku akimchukua mwanaye huyo ambaye kwa sasa analelewa na mama wa Nay.
CREDIT:GPL

No comments: