Maadhimisho ya siku ya mtoto Mkoani Iringa yalifanyika kwenye ukumbi wa CCM ambapo kauli mbiu mwaka huu ni UBAKAJI NA ULAWITI KWA MTOTO VINAEPUKIKA: CHUKUA HATUA KULINDA MTOTO. Kasesela aliyataja maeneo ambayo bado ni hatarishi kwa watoto, shuleni, majumbani na mtaani ambapo majanga haya ya kubaka na kulawiti watoto yamekuwa yakitokea. Ni muhimu wazazi sasa wakasimama kidete kuhakikisha mambo haya yanatokomezwa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bwana Jolwika Kasunga alikemea mtindo wa kuwafundsha watoto nyimbo na dansi zisizo na staha. " Kuanzia leo napiga marufuku watoto kucheza miziki isiyo na staha shuleni, mwalimu atakaye wafundisha atakiona cha mtema kuni".
katika hafla hiyo mtoto yatima Patrick ambaye aliokotwa na mbwa akiwa kwenye mfuko wa plastic toka jalaalni na kuletwa kwenye nyumba ya mtui alizawadiwa kadi ya Bima ya Afya bure kwa miaka 3. Mtoto huyo mwenye miezi 8 analelewa na afisa maendeleo ya jamii. Patrick alinyweshwa chanjo ya vitamin A na mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ambaye alimbeba karibu siku nzima wakati wa sherehe hizo. Nyimbo na ngonjera mbalimbali ziliimbwa na JKT Mafinga pamoja na shule mbalimbali za Mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment