ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 16, 2016

WATU WANAOSADIKIKA KUWA MAJAMBAZI WAIBA MILIONI 100 KATIKA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA

Watu wasiojulikana wamevamia duka la Chase Bureau De Change linalotoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni, mali ya Ashraff Khan na kuiba milioni 100 huko wilayani Moshi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana, baada ya wezi hao kuvunja dirisha la chuma na kuingia sehemu ya kutunzia fedha na kufanikiwa kuiba shilingi za Tanzania, Kenya, na Euro (jumla milioni 100), huku mlinzi wa zamu wa duka hilo akitoweka na kuelekea kusikojulikana.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, huku akitoa taarifa za kuwepo kwa wizi kama huo dukani hapo mwaka 2005, ambapo amesema watu wenye silaha walivamia duka hilo na kupora milioni 44 mchana wa saa sita.

Aidha, kamanda Mutafungwa, amebainisha kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwepo kwa dalili za njama za ndani zinazojumuisha kutoonekana kwa mlinzi sehemu ya tukio, huku akiongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea dhidi ya tukio hilo.

CHANZO: JAMII FORUMS

No comments: