ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 16, 2016

WAZIRI SIMBACHAWENE AFUTA MASHINDANO YA UMISETA 201, 6ASEMA SERIKALI INASHUGHULIKA NA MADAWATI

Mkuu wa Wilaya ya Temeke - Dar es Salaam, Sophia Mjema (wapili kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari katika Mashindano ya UMISETA ambapo kampuni ya Coca Cola ndiyo walikuwa ni wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016. Hata hivyo Mashindano hayo ambayo yalitarajiwa kuanza Juni 16, 2016, yamefutwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, ili kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kutatua changamoto ya madawati kwenye shule zote nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akikagua wachezaji wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya UMISETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola. Uzinduzi huo ulifanyika May 10, 2016 katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo na burudani mbali mbali. --- Mashindano kwa ajili ya fainali za kitaifa za Copa-UMISSETA ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, na ambayo yalipangwa kuanza kufanyika siku ya leo hadi hapo tarehe 24 Juni 2016 yametangazwa kuahirishwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene."Nikiwa kama waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, natangaza kuyafuta mashindabo ya mwaka huu ya umiseta, ili tuwe na wakati mzuri wa kuwashirikisha wadau katika jitihada za serikali za kuhakikisha shule zetu kote nchini zinakuwa na madawati."

No comments: