ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 21, 2016

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA MAJI AFRIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Mkutano wa Kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Convention Center ,Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge wakati wa Mkutano wa Kumi wa Barazala La Mawaziri wa Maji.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaambia wajumbe wa mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri Afrika kuwa muda umefika wa kuacha kuongea na kuweka mkazo kwenye kutelekeza malengo tuliyojiwekea ya kufikia dira ya maji ya Afrika ya mwaka 2025.Ikumbukwe ya kwamba misaada kutoka kwa wafadhili inakikomo kwa hivyo ni muhimu kwa nchi kujiwekea malengo ambayo miradi hiyo itaendelea kuwepo hata misaada ikifika kikomo.

Ushirikiano katika matumizi ya vyanzo vya maji ambavyo vinapakana na nchi zetu Kuendelea kutumia mipango ya ushirikiano iliyopo kama vile ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa bara la Afrika.Taasisi za kifedha za bara kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika iwe katika mstari wa mbele wa kuunda na kupanga mikakati itakayosaidia ili kuhamasisha upatikanaji vya fedha

aliwaomba kuwa azimio litakalofikiwa litoe muongozo kwa wadau wote wakiwemo washirika wa maendeleo kuhusu namna nchi wanachama wanaweza kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama ili kuweza kufikia dira ya Afrika ya maji ya mwaka 2025 na goli namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu.

No comments: