Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi imeeleza kuwa.
1. BODI YA MAPATO (ZRB)
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 14 cha sheria ya Bodi ya Mapato ya 1996, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Amour Hamil Bakar kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar. Bwana Amour Hamil Bakar anachukua nafasi ya Bwana Abdi Khamis Faki ambae anastaafu kwa mujibu wa Sheria.
Utezi huo unaanza tarehe 1 Agost 2016.
Aidha kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 15(1) (A) cha sheria hiyo kama ilivyorekebishwa na kifungu 11 cha Sheria Namba 2 ya mwaka 2000, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Khadija Shamte Mzee kuwa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar. Bibi Khadija Shamte Mzee anachukua nafasi ya Bwana Hafidh Ussi Haji ambae uteuzi wake umefutwa.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
2.TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Tume ya Maadili ya Umma Namba 4 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Said Bakari Jecha na Bibi Sebtuu Mohammed Nassor kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai, 2016.
3. BODI YA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 11(1)(a) cha Sheria ya Shirika la Magazeti ya Serikali Namba 11 ya 2008, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Umi Aley kuwa Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
4. TUME YA UTANGAZAJI
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Tume ya Utangazaji ya Zanzibar Namba 6 ya 1997, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Dkt. Ali saleh Mwinyikai kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji ya Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
5. BARAZA LA SANAA NA SENSA YA FILAMU NA UTAMADUNI
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na utamaduni Namba 7 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Maryam Mohamed Hamdan kuwa mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.
6. BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Baraza la Mitihani la Zanzibar Namba 6 ya 2012, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Maryam Abdalla Yussuf kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
7. SHIRIKA LA VIWANGO LA ZANZIBAR (ZBS)
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8(2)(a) cha Sheria ya Shirika la Viwango la Zanzibar Namba 1 ya 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua tena Profesa Ali Seif Mshimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.
No comments:
Post a Comment