Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amegawa mikakati na majukumu ya kazi kwa watendaji wa halmashauri na wenyeviti wa serikali za mitaa, huku akiwaonya waliokuwa wakiishi kwa kutegemea rsuhwa kujisogeza mapema au kutubu madhambi yao.
Lyaniva alisema hayo juzi alipokutana na watendaji wa halmashauri hiyo na wenyeviti wa Serikali za mitaa, alitoa wiki mbili kwa wakuu wa idara na watendaji hao kuondoa kero zinazowakabili wananchi, ikiwamo migogoro ya ardhi.
“Kila mmoja achukie rushwa kutoka moyoni mwake, tukifanikiwa kukomesha naamini wilaya yetu itakuwa na maendeleo makubwa,” alisema Lyaniva.
Alisema watendaji wanaofanya kazi kwa kutegemea rushwa waanze kujiondoa kabla hawajachukuliwa hatua na kutafuta sehemu nyingine ya kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment