Mkuu wawilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akisoma taarifa ya wilaya kwa Naibu waziri Mh Jafo (kulia) Katibu tawala Bwana Joseph Chitinka ( Kushoto) akisililiza
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Mh Stephen Mhapa ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa ALAT akimpokea Mh Jafo ukumbi wa siasa ni kilimo
Mh Selemani Jafo na Mheshimiwa Richard Kasesela wakishirki katika uzinduzi wa sehemu ya kunawia watoto katika shule ya Mikongati
maji kwa hiasani ya UNICEF walifadhiri mradi wenye thamani ya Tshs Mil 119 kwa kijiji cha Mikongati
maji kwa hiasani ya UNICEF walifadhiri mradi wenye thamani ya Tshs Mil 119 kwa kijiji cha Mikongati
Mfadhiri wa mradi wa Maabara katika zahanati ya Kisinga Bwana Feisal ASAS akipokea cheti cha shukrani toka kwa naibu waziri
Akimkaribisha Naibu waziri, Mheshimiwa Kasesela aliomba seriakli kuharakisha fedha ili kukamilisha miradi ya maji na barabara, pia kuomba uwezekano kila barabara zinapo jengwa yatengwe maeneo kwa ajili ya emergence unit ili kuokoa miasha ya watu mara ajali zinapotokea. aliendelea " leo Mh waziri umezindua maabara hapa Kising'a lakini eneo hili lipo barabara kuu ya kuelekea Dodoma ajali zinapotokea tunapata tabu sana kuokoa maisha ya wananchi ni muhimu sasa tanroads wana disign barabara mpya ziwepo pia fedha za kujenga vituo vya dharura ambavyo vyawezwa kuunganishwa na vituo vya kupumzikia wananchi ili halmashauri zetu zipumue mara yatokeapo majanga".
Pia akiongea kwenye mkutano wa watumishi Mkurugenzi wa halmashauri Bwana Robert Munyusi pamoja na Katibu tawala wilaya ya Iringa Bwana robert Chitinka wote kwa pamoja walimpongeza Naibu waziri kwa kasi kubwa ya utendaji kazi wake.
Ziara ilimalizika kwa kumtembelea Mwalimu aliye fiwa na mwanae wakati ziara ikiendelea. Naibu waziri aliwafariji wafiwa na kutoa ubani kisha kuendelea na safari kuelekea Dodoma.
No comments:
Post a Comment