Friday, August 5, 2016

CHADEMA WALAANI UKANDAMIZAJI WA POLISI

Katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji

Katibu Mkuu wa Chadema, Vicent Mashinji, amesema amelipokea kwa huzuni kubwa na kufedheheshwa kile alichokisema kama hali ya kukosekana kwa ustaarabu katika taifa.
Ameyasema hayo akiongea na waandishi wa habari baada ya sakata la Tundu Lissu na polisi ambalo linaendelea.
“Jeshi letu la polisi limekuwa chombo cha ukandamizaji na kuondoa staha katika jamii. Aibu hii ni kubwa mno kwa Watanzania kuweza kuivumilia. Ni fedheha kubwa kwa jeshi letu linaloongozwa na wanasheria waliobobea kufanya mambo nje ya misingi ya sheria,” alisema Mashinji.
“Mh. Tundu Lissu ni mnadhimu wa kambi ya Upinzani Bungeni, ni Wakili Msomi anayeheshimika duniani pote, ni Mbunge anayewakilisha jimbo na ni Mtanzania,”,alisisitiza.
“Siamini kwamba polisi wangemtaka afike kituo chochote cha polisi angeweza kukaidi, lakini wameamua kumkamata na kumsafirisha kama mnyang’anyi. Aibu hii ni kubwa sana na sidhani kama itafutika machoni pa jamii yetu.”
Hata hivyo amewashukuru vijana wote waliojitoa kumsindikiza kwa kusafiri na polisi toka Singida kuja Dar na pia alisema kuwa, “Huu ni ujumbe tosha kwa jeshi la polisi.”
BY: EMMY MWAIPOPO

1 comment:

  1. Wananchi hatuli siasa. Tunataka tukienda kwenye Ofisi za Serikali tunapata huduma tunayotaraji. Magufuli anayafanya hayo. Kwanini wapinzani wasimuunge mkono. Hapa wengine wanatafuta kula yao tu

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake