IKIWA ni siku kadhaa baada ya mwanamuziki Koffi Olomide kufukuzwa nchini Kenya kwa kumpiga mnenguaji wake, Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Rhumba, raia wa Jamhuri ya Kidemokasia ya Kongo, Defao Matumona ‘General Defao’ leo amezuiliwa kwenye hoteli moja iliyopo mjini Mombasa nchini Kenya baada kushindwa kulipa bili kiasi cha Ksh 20,000.
Defao ameshindwa kulipa pesa hiyo baada ya kuongeza muda wa kuendelea kuishi kwenye hoteli hiyo ambayo alitakiwa aondoke juzi Alhamisi japo aliomba kuongezewa muda wa siku mbili kuanzia mpaka leo Jumamosi, Agosti 6 ambapo ameshindwa kulipa na kujikuta akishikiliwa kwa tuhuma hizo.
Inasemekana promota wake ajuliakanaye kwa jina la Rashid Osundwa ndiye aliyempeleka Kenya kufanya shoo nchini humo na ndiye aliyeshimwachia msala huo.
Defao amesema Osundwa alimpeleka Mombasa kufanya shoo Jumamosi, Julai 30, kwa makubaliano ya kulipwa Ksh 90,000 kwa shoo hiyo.
“Nilitakiwa kuondoka kwenda Nairobi Alhamisi [Agosti 4] l lakini Rashid alimwambia abaki ili afanye shoo nyingine Jumatano,” Defao amesema leo.
Hakufanikiwa kufanya shoo siku ya Jumatano alipojaribu kuwasiliana na viongozi walioandaa shoo hiyo hawakupatikana wala hawakufika kabisa. Defao alitakiwa pia kulipwa Ksh90,000 kwa ajili ya shoo ya Jumatano lakini hakulipwa.
Jitihada zilifnyika kumsaka Osundwa ili azungumzie sakata hilo lakini simu yake ilikuwa imezimwa wakati viongozi wandamizi wa Osundwa hawakutaka kuzungumzia suala hilo.
Defao anadai amekosa kufanya shoo ya Nairobi iliyokuwa ifanyike jana Ijumaa.
CHANZO: the-star.co.ke kwa masaada wa GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake