Sunday, August 7, 2016

TGNP NA ACTION AID WAKUTANISHA WANAWAKE NA VIONGOZI KUJADILI USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA NAFASI ZA MAAMUZI

Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi, Bi. Bengi Issa akizungumza jambo wakati wa kuzindua mjadala wa wadau uliowakutanisha wanawake viongozi ulioandaliwa na TGNP Mtandao pamoja na Action Aid Tanzania.(Picha na Geofrey Adroph)
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mwanaharakati wa haki za mwanamke, Mh. Anne S. Makinda akizungumza jambo wakati wa kujadili nafasi ya mwanamke na uongozi iliyoandaliwa na TGNP Mtandao na Action Aid Tanzania.
   Mwenyekiti wa kitaifa wa chama kipya cha siasa, ACT – Wazalendo na Mwanaharakati wa maendeleo ya Mwanamke, Anna Mghwira akizungumza jambo wakati wa kujadili na kutoa tamko kuhusu nafasi ya wanawake na uongozi iliyofanyika katika ukumbi wa SeaShell jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi, Bi. Bengi Issa(wa pili kutoka kushoto) akipokea tamko kwa kutoka kwa Mwajuma Nuty lililosomwa na wawakilishi wa wanawake viongozi.Wa kanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi 
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka TAKUKURU, Neema Mwakalyelye akizungumza na wanawake viongozi kuhusu mchango wa TAKUKURU katika kupunguza rushwa hasa rushwa ya kingono inayoshamiri sana maofisini na hata katika ngazi mbalimbali za uongozi.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kinachoendelea katika mjadala wa Wanawake na Uongozi ulioandaliwa TGNP Mtandao pamoja na Action Aid Tanzania

Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis 'Gadafi' aichangia mada

Vikundi vya burudani vikitoa burudani wakati wa kujadili

Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake