Friday, August 5, 2016

UHAMIAJI YAWAKAMATA RAIA WAWILI WA KIGENI WAKIFANYA KAZI SERIKALINI

Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi ambaye alikuwa Mganga Mkuu katika kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa kufanya kazi Serikalini wakati si raia wa Tanzania.

Idara ya Uhamiaji nchini imewakamata Watu wawili ambao sio raia wa Tanzania, waliokuwa wakifanya kazi serikalini
Bahilanya Milingita (Congo) alikuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Mwingine ni Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba (Malawi) ambaye alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya Mburahati.

Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo ambaye anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kinyume na sheria za nchi.

7 comments:

  1. Kwa mtizamo wangu huyu jamaa hana kosa...uzembe wa idara zetu na rushwa ndicho chanzo cha kuwa na watu kama hawa. 1986-2016? Sidhani kama hata kwao anakukumbuka.

    ReplyDelete
  2. Tangu mwaka 1986 mpaka leo, uhamiaji, na mwajiri wake Tanesco walikuwa wapi? Inabidi jamaa apewe uraia tu (under humanitarian basis). Miaka thelasini ameisha jenga familia na watoto wake ni watanzania period.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tanzania bana...kwahiyo unatetea uvunjifu wa sheria?

      Delete
    2. Apigwe fine yaishe! Nadhani huyu ni Mtanzania kwa moyo hata kama kimakataratasi sio Mtanzania!

      Delete
  3. Itabidi apewe uraia, kama hajafanya au hana criminal record, makosa ni ya utaratibu wetu, na uhamiaji na home land security kwa waliokaa nje ya nchi wanaekewa naongelea nini,?ina maana idara zote zilikuwa zimelala,?

    ReplyDelete
  4. Serikali ya bongo bwana SMH,hapo uhamiaji inahusika na waajiri wao pia,wapeni tu uraia waendelee kuchapa kazi

    ReplyDelete
  5. Strengthen our immigration law like any other country, viongozi was Nyman didn't work right Kwa ajili ya corruption but this time kila mtu afuate sheria. Angalia nchi nyingine watanzania ambao wako illegal wanavyoteseka. Please give a credit.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake