Laudit Mavugo akisani mkataba ya kuitumikia klabu hiyo akiwa na Rais wa Simba Evans Aveva.
Fredric Blagnon akisani mkataba ya kuitumikia klabu hiyo.
Janvier Bokungu (kushoto) akikabidhiwa jezi.
Rais wa Simba Evans Aveva akimkabidhi jezi Musa Ndusha.
KLABU ya Simba sasa imeamua kukamilisha kila kitu kabla ya kuanza kwa msimu wa 2016/17 ambapo jana iliamua kumalizana na wachezaji wake wote wa kimataifa.
Hatua hiyo imekuja siku moja kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili ambapo sasa klabu hiyo imekamilisha usajili wa wachezaji wote saba wa kimataifa huku ikiachana na Mghana, Aboagye Gerson.
Wachezaji ambao walikamilisha usajili kwa kusaini mikataba ya kuitumikia klabu hiyo, jana jioni ni Fredric Blagnon raia wa Ivory Coast, Laudit Mavugo (Burundi), Janvier Bokungu, Musa Ndusha (wote DR Congo) na Method Mwanjali (Zimbabwe).
Wachezaji hao walisaini mikataba hiyo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Collins Frisch.
Wachezaji hao watano wanaungana na wengine wawili ambao walikuwepo kikosini hapo msimu uliopita, Vincent Angban wa Ivory Coast na Juuko Murshid wa Uganda.
No comments:
Post a Comment