Monday, August 8, 2016

WATUMISHI WASAINISHWA SAA TISA USIKU MKESHA WA MWENGE

Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza
By Suzan Mwillo na Daniel Makaka, Mwananchi ;mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar/Sengerema. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Magessa Boniface amesema atawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa wilaya watakaoshindwa kuhudhuria mkesha wa Mwenge usiku wa kuamkia leo.

Katika kutimiza azma hiyo, Magessa alisema, “Mtatakiwa kujiandikisha kwa kila idara saa 6.00 usiku, saa 9.00 usiku na saa 12.00 asubuhi, ambaye hatakuwepo atahesabika kuwa ni mtoro na atachukuliwa hatua za kinidhamu.”

Katika tangazo hilo alililotoa jana kwa watumishi hao, mkurugenzi huyo alisema watumishi wote wa wilaya hiyo wanatakiwa kuwapo katika mkesha huo bila kukosa. Pia, aliagiza kila mtumishi kutia saini mara tatu kuthibitisha ushiriki wake. Mwenge uliingia wilayani humo jana Agosti 7 na kukesha viwanja vya Shule ya Msingi Sengerema.

Akizungumzia tangazo lake lililobandikwa maeneo mbalimbali wilayani humo, Magessa alisema alilazimika kutoa agizo hilo kukomesha tabia ya baadhi ya watumishi kufika kwenye mkesha wa Mwenge na kuondoka kurejea majumbani mwao.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake