Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi fedha taslimu
Shilingi 1,119,000, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa
Huruma kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa ajili ya
kusaidia majukumu mbalimbali ya ulezi wa watoto hao. Fedha hizo
zilitolewa na Masauni pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo kwa lengo la
kusaidia kituo hicho. Pia Baraza hilo lilitoa mchele gunia moja, kilo
50 za sukari, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na
fulana 100. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimkabidhi misaada
mbalimbali, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma
kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa ajili ya kusaidia
watoto hao. Pia Masauni alimkabidhi msimamizi huyo wa kituo mchele
gunia moja, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11, fulana 100
pamoja na fedha taslimu Shilingi 1,119,000 ambazo zilitolewa na
wajumbe wa Baraza hilo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba mtoto) na Katibu wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga
(kulia) wakiwa na baadhi ya watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma
cha mjini Geita, mara baada ya Masauni kukabidhi fedha taslimu
shilingi 1,119,000 pamoja na vyakula kwa kituo hicho ambapo misaada
hiyo ilitolewa na Baraza la Usalama barabarani ambalo linaadhimisha
Wiki ya Nenda kwa Usalama mjini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Watoto
Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma kabla ya kuwakabidhi misaada
mbalimbali ambayo aliwaongoza Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani kukusanya misaaida mbalimbali. Misaada hiyo iliyotolewa ni
fedha taslimu shilingi 1,119,000 pamoja na mchele gunia moja, kilo 50
za sukari, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na
fulana 100. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba mtoto), Mkuu wa Mkoa
wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kulia kwa Masauni),
pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wakiwa
katika picha ya pamoja na Watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma
cha mjini Geita, wakati Mwenyekiti huyo wa Baraza pamoja na wajumbe
wake kukitembelea kituo hicho na kukabidhi misaada mbalimbali. Tukio
hilo lilifanyika mara baada ya Masauni kuizindua Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani ambayo inaadhimishwa Kitaifa mjini Geita. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.( PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).
No comments:
Post a Comment