Siku kadhaa baada ya Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm kuandikia uongozi wa klabu barua ya kujiuzulu kuendelea kuifundisha klabu hiyo, hatimaye uongozi wa Yanga umuandikia barua ya kumuomba kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Katika barua ambayo imeandikwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit imeeleza kuwa Yanga inafahamu kwa kiasi gani ameisaidia klabu hiyo kwa kipindi ambacho amekuwa akiifundisha na inapenda kuona akiendelea na nafasi yake ya ukocha kama ilivyokuwa awali.
No comments:
Post a Comment