Dodoma/ Dar es Salaam. Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekiri kuingia mkataba wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco Village, Kigamboni na kampuni ya Azimio Housing Estates (AHEL) ambayo haikuwa na mtaji hali iliyolazimu kusitisha mradi huo huku likihofia kupata hasara ya Sh270 bilioni.
Machi mwaka huu, Mwananchi liliandika “NSSF yaliwa mchana kweupe” likifafanua ufisadi katika mradi huo na mingine ya Mwanza, Pwani, Mtwara na Arumeru, Arusha ambako ekari moja ya ardhi ilithaminishwa kwa Sh1.8 bilioni.
Jana, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, akitoa taarifa ya kusimama kwa mradi huo kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema wanahofia kupoteza Sh270 bilioni kutokana na kushirikiana na mbia ambaye hakuwa na fedha.
Profesa Kahyarara aliwaambia wajumbe wa PAC kuwa mradi wa Kigamboni ulisimama tangu Februari na kwamba juhudi zinafanyika kuhakikisha mbia huyo AHEL anarejesha fedha hizo.
No comments:
Post a Comment