|
Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
|
11, Oktoba, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI YA
MAREKANI YAWEZESHA MAZUNGUMZO YA MOJA KWA MOJA KATI YA WASICHANA 50 WA
KITANZANIA NA MKE WA RAIS MICHELLE OBAMA KUHUSU ELIMU KWA WASICHANA
Katika kuadhimisha Siku ya
Kimataifa ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike hapo tarehe 11 Oktoba, wawakilishi
Serikali ya Marekani na wale wa Shirika la Plan International waliungana na Mke wa Rais wa Marekani
Michelle Obama, Mwanamuziki Mahiri wa Kitanzania Vanessa Mdee na Wasichana wa
Kitanzania 50 katika mjadala maalumu kuhusu
umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.
Mama Michelle Obama aliongoza
mjadala uliopewa kichwa kisemacho “Mstakabali Mwema: Mjadala wa Kimataifa
kuhusu Elimu kwa Mtoto wa Kike,” ulioandaliwa na mradi wa jarida maarufu la Glamour wa kuwasaidia wasichana na
kuwashirikisha wasichana kutoka nchi mbalimbali duniani. Akishiriki kutokea
Washington DC, Mama Obama aliungana na mwigizaji na mwanaharakati Yara Shahidi
pamoja na Mhariri Mkuu wa jarida la Glamour
Cindi Leive. Kwa kupitia Mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao
(video-chat)wasichana kutoka Tanzania, Jordan, Peru, Uingereza na Marekani
walijadili changamoto zinazowakabili na namna ya kuzikabili ili waweze kupata
elimu bora. Wasanii mashuhuri kutoka katika nchi hizo walishiriki katika
majadiliano hayo, ambapo nchini Tanzania mwimbaji mahiri Vanessa Mdee aliongoza
kipindi cha maswali na majibu kati ya wasichana wa Tanzania na wale wa nchi
nyingine.
“Wasichana wa Tanzania
wanastahili kupata kila fursa ili waweze kufikia upeo wa uwezo wao,” alisema
Mdee. “Nina hamasa kubwa mno ya kusaidia elimu yao na ninashukuru kuwa sehemu
ya tukio hili la kuonyesha nini Tanzania na nchi nyingine zinaweza kufanya
katika kuwaandaa wasichana kufanikiwa shuleni na hata baada ya kuwa wamemaliza
masomo yao.”
Tanzania ni moja kati ya nchi
mbili za kipaumbele katika mpango ujulikanao kama “Let
Girls Learn” uliozinduliwa na Rais Barack Obama na Mama Michelle
Obama hapo mwaka 2015 kwa lengo la kushughulikia changamoto mbalimbali
zinazowakwamisha wasichana kupata elimu bora itakayowawezesha kufikia upeo wa
uwezo wao.
Akiwakaribisha washiriki wa
Kitanzania katika majadiliano hayo Mkurugenzi wa Shirika la Marekani la
Maendeleo ya Kimataifa Sharon Cromer alisisitizia umuhimu wa kuhakikisha kuwa
kila msichana wa Kitanzania anapata elimu bora.
“Wanawake na vijana ndio
kitovu cha jitihada zetu za kuisaidia Tanzania kuwa imara zaidi, yenye ustawi
zaidi na iliyo jumuishi zaidi,” alisema Cromer. “Ni lazima tufungue fursa na
uwezo wa wasichana kama hawa waliopo hapa leo iwapo kweli tunataka kuinua hali
ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania na kuinua fursa kwa Watanzania wote.”
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake