ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 27, 2016

UBALOZI WA UJERUMANI WACHANGIA TAMASHA LA BUSARA ZANZIBAR 2017.

Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said akitiliana saini ya Makubaliano ya kusaidia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar na Balozi wa Ujerumani Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani imekubali kuchangia  €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 12,hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyyat Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali wanaotembelea Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi  Egon Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini ya makubaliano ya kuchangia Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar, leo mchana. 

No comments: