ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 26, 2016

Unyang’anyi wamtupa jela miaka 30

By Faustine Fabian, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Maswa. Unyang’anyi wa Sh450,000, simu ya mkononi aina ya LG yenye thamani ya Sh300,000 na kadi ya Benki ya NMB umemtupa jela miaka 30 kijana mkazi wa Mtaa wa Biafra ‘B’ mjini Nyalikungu, wilayani Maswa.

Mshtakiwa Juma Abdallah (20), amehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama ya Wilaya ya Maswa baada ya kutiwa hatiani kwa unyang’anyi wa kutumia silaha alioutenda kwa mfanyabiashara Simon Edward.

Hukumu ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Tumaini Marwa. Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Nassib Swedy alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Mei 21, kwenye Mtaa wa Unyanyembe mjini Maswa.

No comments: