Mtaribu wa tamasha la 'Kale ni
Dhahabu' ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina Kaphipa
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na tamasha la
utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania. Pamoja nae ni Afisa Masoko, Anael Masasi
Mtaribu wa tamasha la 'Kale ni
Dhahabu' ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina Kaphipa
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na tamasha la
utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania. Pamoja nae ni Afisa Masoko, Anael Masasi (kushoto) na Msemaji wa Tamasha hilo, Juma Mwajacho (kulia) pamoja na Mke wa Chief.
Mtaribu wa tamasha la Kale ni Dhahabu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina Maro akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu tamasha la utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania.
Sabina Kaphipa akicheza ngoma na wasanii wa Kundi la sanaa Makumbusho.
Juma Mwajasho ambaye ni msemaji wa tamasha hilo (kulia) akizungumza.
***************
SEREEE Company Inayo furaha kuandaaa Tamamsha la
kiutamaduni wa Mtanzania linaloitwa CHAKALE DHAHABU, kwa lengo kuu la kudumisha tamaduni zetu na kufanya
jamii ya Kitanzania kuishi kwa kufurahia utamaduni wake.
SEREEE Company
inaandaa tamasha la kwanza la CHAKALE DHAHABU ambalo litafanyika katika jiji la Dar es salaam, litakua ni
tamasha la siku nzima ambalo litafanyka katika viwanya vya Uhuru( Uwanja wa
Taifa tarehe 3 December na kufuatiwa na
tukio jingine siku ya tarehe 4 december ambapo kutakua na chakula cha jioni
katika hoteli ya Golden Tulip Dar es salaam.
CHAKALE DHAHABU inalengo la kuwa ni tamasha
ambalo litakua likifanyika kila mwaka likizunguka katika mikoa tofauti ndani ya
nchi ya Tanzania.
CHAKALE DHAHABU ni Tamasha lililo beba utamaduni
wa kitanzania ambapo makabila yoye yatashiriki pamoja na machifu wao, Tamamsha
litalinda na kuendeleza utamaduni wa mtanzania na Africa kwa ujumla.
Tamasha limegawanyika katika burudani na
shughuli mbalimbali za kiasili kama muziki,Ngoma,Chakula,Vinywaji,Mashairi,Hadithi,Matambiko
pamoja na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za kiasili. Zinazotengenezwa hapa
Tanzania.
Seree Company ni kampuni ya Kitanzania inayokua
haraka katika nyanja ya juandaa na
kusimamia burudani na Matamasha kwa
mfano, Harusi,Sherehe za kifamilia,Sherehe za makampuni, na sherehe za
Kiserikali. Dira yetu ni kuwaunganisha pamoja wazee,vijana na wazazi katika
nyanja ya sanaa na utamaduni wetu ambao kwa namna moja au nyingine unaendelea
kufifia.
Tamasha litafanyika kwa monyesho kama ifuatavyo
MACHIFU
Machifu hawa ni viongozi wa kimila ambao ndio
chimbuko la utamaduni wa Mtanzania
walikuwepo kabla tawaza za kiserikali kuwepo walisimamia na kuziendesha koo pamoja
makabila, nafasi ya machifu katika tamasha la CHAKALE DHAHABU ni kutoa elimu
kwa jamii kuacha kabisa tabia ya kuwauwa vikongwe na maalbino pia watatuonyesha
jinsi matambiko yalivyokua yakifanyka kwa lengo la kukumbuka na kuielimisha
jamii nzima ya watanzania.
BURUDANI
Patakua na Burudani ya muziki wa asili pamoja na ngoma toka katika makabila tofauti
ya Tanzania, pia patakua na hadithi toka kwa wasimulizi mahiri toka hapa
Tanzania pamoja ma mashaishi toka kwa
malenga wetu.
VYAKULA
Kutakua na vyakula vya aina tofauti kutoka
katika makabila tofauti ya Tanzania.
Sereee campany inatoa shukrani za dhati kwa
waandishi wa habari kwakua kupitia nyie Tamasha hili litakua na
mafanikio .
No comments:
Post a Comment