ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 5, 2016

KASESELA AWASHUKURU EPIC KWA MSAADA WA MAJI LUPALAMA

Dc kasesela akikata utepe katika uzinduzi wa Bomba la maji katika kijiji cha lupalama kulia kwake ni bwana Johnson Kisinda muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Kushoto ni Diwania wa Lupalama.
Dc Kasesela alikuwa wa kwanza kukinga maji katika Bomba la kijiji.
Dc kasesela akimtwisha Maji bi Theobadina Sengailo.
Wanakijiji wa lupalama wakisikiliza jambo kutoka kwa mkuu wa wilaya.
Wanakijiji wa lupalama wakisikiliza jambo kutoka kwa mkuu wa wilaya.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amezindua mradi wa maji katika kijiji cha lupalama kilichopo katika Tarafa ya kalenga Wilayani Iringa, Mradi huo umedhaminiwa na Shirika la E.P.I.C (Everyday People Initiate Changes) la Marekani liloanzishwa na Mwanamuziki wa Marekani Tinara Moore. Ambaye aliwahi kutembelea Tanzania na baadae kuamua kutoa misaada mbalimbli.

Wanakijiji wa Lupalama kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji, “Tulikuwa tukilazimika kutembea saa zima kufata maji mtoni nabado maji haya kuwa ya uhakika kwa maana kipindi cha kiangazi mto ulikuwa una kauka jambo lililopelekea kupata shida kubwa sana katika upatikanaji wa maji” anaeleza Bi Theobadina Ngailo mkazi wa Lupalama anaongeza kuwa “Tulikuwa tunatumia hata maji ya kwenye vidimbwi ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu kwani muda mungine tulikuwa tukichangia maji hayo na mifugo jambo lilipolekea kulipuka kwa magonjwa kama kuhara”.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo Muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Bwana Johnson Mkini Kisinda amsema kuwa mradi huo umeghalimu pesa zaidi ya milioni therasini na tano hadi kukamilika “Hiki ni kisima cha pili kwa urefu katika visima vyote tulivyo chimba kwani Lengo lilikuwa kuchimba mita sabini tu ila tulikosa maji tukalazimika kuchimba mita mia moja na themanini kwenda chini hadi kuyafikia maji”, pia ame waasa wanakijiji wa Lupalama kuwa walinzi wa miundo mbinu hiyo ya maji kwani ni kwa faida yao wenyewe.

Akikabidhi Mradi huo kwa wanakijiji wa lupalama mkuu wa wilaya ya Iringa amewaomba wana kijiji hao kuusimamia vema mradi huo kwani Ofisi yake ina mpango wa kuhakikisha maji hayo yana sambazwa katika Maeneo Yote ya kijiji hicho ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wingi “Ni ndoto yangu kuona Maji haya yana wafikia wanakijiji wote wa lupalama ikibidi na maeneo ya Jirani wapate pia maji haya nitoe agizo kwa serikali ya kijiji kuunda kamati ya kusimamia na kutunza mradi huu ili uendelee kufanya kazi na kunufaisha wengi wakati mimi niki hangaika kuona jinsi gani tunapata pampu ya Umeme ikishindikana hata ya kutumia nguvu ya jua ili tusambaze maji haya sehemu nyingi zaidi”.

Pia ameagiza Serikali ya kijiji Kuanza mara moja Mchakato wa ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo kwani ni kero ya muda mrefu hasa kwa akina mama kwani wana lazimika kutembea kilomita saba kufuata huduma ya afya “Nawaombeni Zoezi hili lianze mapema sana na ikibidi kila mwanakijiji ashiriki kukusanya mawe ya ujenzi na pindi mkiwa tayali ujenzi uanze mara moja”.

Katika hotuba yake Mkuu wa wilaya pia amehimiza watu kutunza chakula “ mvua mwaka huu sio za kuridhisha hivyo basi ipo hofu ya kukosekana chakula ni muhimu wananchi wakatunza chakula na kulima mazao yenye kuhimili ukame”

No comments: