Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya viongozi wa vyama vya michezo leo mkoani Mbeya (hawapo pichani) ikiwa ni moja ya malengo ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Kulia ni Kaimu Afisa Michezo mkoa ambaye pia ni Afisa Michezo Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya viongozi wa vyama vya michezo leo mkoani Mbeya . (Picha na Eleuteri
Mangi-WHUSM, Mbeya)
Na Eleuteri
Mangi-WHUSM, Mbeya
Wadau wa michezo
mkoni Mbeya wametakiwa kuendeleza mshikamano walionao ili kuifanya sekta ya
michezo kuwa chanzo cha kuongeza fursa za ajira kwa vijana pamoja na wataalamu
wengine wa michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema hayo leo
jijini Mbeya alipokuwa akiongea na baadhi ya viongozi wa vyama vya michezo
mkoani humo ikiwa ni moja ya malengo ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
“Nimefurahishwa na
mkoa wa Mbeya kuwa na mipango ambayo imewafanya vyama vya michezo kuendeshwa
bila kuwa na migogoro, hii ni hatua nzuri imenipa moyo, mkishikamana vizuri
mtafanikiwa sana katika malengo yenu ya michezo” alisema Prof. Ole Gabriel.
Ili kuhakikisha
michezo inakuwa na tija kwa mkoa wa Mbeya na taifa, Prof Ole Gbriel ametaka
viongozi hao kuwa na mkakati wa kimkoa wa kubadilisha fikra za watu katika
michezo na kutambua kuwa zipo fursa nyingi katika michezo yote bila kubagua
aina ya mchezo.
Awali akitolea
ufafanuzi baadhi ya masuala ya michzo, Prof. Ole Gabriel ameataka wadau hao kutambua
kuwa michezo inaanzia katika ngazi ya chini, hivyo ni wajibu wao kuendeleza
michezo kwa kubadili fikra za wazazi, vijana, walezi kuipenda michezo kwa kuwa
inamchango mkubwa katika ajira, pato la familia pamoja na uchumi wa taifa.
Akimkaribisha Katibu
Mkuu Prof. Ole Gabriel, Kaimu Afisa Michezo mkoa ambaye pia ni Afisa Michezo
Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba amesema kuwa Serikali ya mkoa inaendelea
kushirikiana na wadau wa michezo yote kwa kuzingatia michezo ni ajira, udugu
katika kujenga umoja wa michezo kimkoa na taifa.
Akizunguzia mpira wa
miguu, Katibu Msaidizi Chama cha Mpira wa Miguu Mbeya (MREFA) Lucas Kubaja
amesema kuwa mpira wa miguu unachezwa kuanzia ngazi ya chini, wilaya zote hadi
mkoa.
Kubaja ameongeza kuwa
mkoa unapokuwa na timu nyingi za michezo mbalimbali katika ligi za michezo hiyo
inasaidia kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mkoa wa mbeya kunapokuwa na
timu zinazokuja kucheza mechi zao kwenye ligi husika.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti wadau hao wa michezo wamemweleza Katibu Mkuu mwenye dhamana ya michezo
kuwa michezo mingi mkoani Mbeya inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na
viwanja vya michezo hatua ambayo inarudisha nyuma ukuaji wa michezo mbalimbali.
Vyama nya michezo vilivyoshiriki
mkutano huo huo ni mpira wa miguu (MREFA), mpira wa pete (CHANETA), mpira wa
kikapu, chama cha makocha, riadha, vishale pamoja na pool table.
Aidha,katika ziara
hiyo, Katibu Mkuu pia ametembelea Ofisi za kanda ya Nyanda za Juu Kusini za Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
kwa lengo la kujionea namna wanavyofanya kazi ya kuimarisha mawasiliano katika
kanda hiyo.
No comments:
Post a Comment