Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (wapili kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimshukuru Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Balozi huyo alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke nje ya jengo la Wizara hiyo, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Balozi huyo alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza. Kulia ni Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.
Waziri Mwigulu alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Mwigulu.
Hata hivyo, Balozi Sara alimshukuru Waziri Mwigulu kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania.
Pia kikao hicho kiliudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira pamoja na Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
No comments:
Post a Comment