Thursday, December 29, 2016

BONDIA FRANCIS CHEKA ASHIKILIWA NA POLISI MKOANI MOROGORO

Bondia Francis Cheka ashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 28

Bondia huyo ambaye yuko rumande kwa sasa, anakabiliwa na kosa la kukataa kupanda ulingoni Desemba 25 dhidi ya Bondia Abdallah Pazi (Dulla Mbabe)

Kwa mujibu wa Promota wake, Kaiki Siraji, akifungua kesi katika Kituo cha polisi cha Kawe kwakuwa Cheka alimbadilikia dakika za mwisho wakati walikuwa na makubaliano kimkataba ulio kwa mujibu wa sheria za ngumi


Hata hivyo, Bondia Cheka atapelekwa Dar es salaam kesho akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kesi hiyo katika kituo cha Kawe ambako kesi ilifunguliwa Desemba 25.

Chanzo: Mtanzania

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake