Wednesday, December 28, 2016

POLISI WAMNASA MUUGUZI KWA WIZI WA DAWA ZA SERIKALI MKOANI KIGOMA

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia wakazi wawili wa kijiji cha Kaguruka kata ya Rungwe Mpya wilayani Kasulu akiwemo muuguzi wa zahanati ya kijiji hicho wakituhumiwa kuiba dawa za serikali zilizoletwa katika zahanati hiyo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi FERDINAND MTUI amesema watu hao ambao majina yao yamehifadhi , walishtukiwa na wananchi baada ya muuguzi huyo kuiba na kumkabidhi mwananchi mwingine kwa lengo la kuficha.

Hata hivyo wananchi walibaini wizi huo na kuanza kuwashambulia mpaka viongozi wa kijiji walipofika na kuwafungia watuhumiwa ofisi ya kijiji ili kunusuru maisha yao.


Kamanda MTUI amesema watuhumiwa hao walikuwa wameiba dawa za aina mbalimbali za binadamu na vipimo vya malaria ambavyo thamani yake haijafahamika na kwamba watafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake