Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe ikicheza ngoma ya Limdoya wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
Wasanii kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe wakicheza ngoma ya Limdoya wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wanyakazi Januari 25, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha chai cha Lupembe, Mussa Kefa (kushoto kwake) wakati alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wafanyakazi akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment