ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 26, 2017

Mexico: Hatutalipia ukuta wa Donald Trump

Image captionRais Enrique Pena Nieto wa Mexico kushoto na mwenzake wa Marekani Donald Trump kulia

Mexico imesema kuwa haitalipia ukuta uliopendekezwa na rais wa Marekani Donald Trump ,kulingana na rais wa taifa hilo Enrique Pena Nieto ambaye ameshutumu mpango huo wa kujenga ukuta.

Hatahivyo rais huyo hakizungumzia kuhusu iwapo atafutilia mbali ziara yake ya Marekani ambapo anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump tarehe 32 Januari.

Trump tayari amesaini agizo la urais la kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico na amesisitiza kuwa Mexico itailipa Marekani kwa ukuta huo.
Trump: Mexico watalipia ukuta '100%'
Trump: Tutajenga ukuta katika mpaka na Mexico
Marekani kujenga ukuta mara moja


Rais Pena Nieto aliambia taifa katika hotuba ya runinga kwamba :Nimesema tena na tena kwamba Mexico haitalipia ukuta huo.

''Ninajuta na kushutumu uamuzi huo wa marekani wa kutaka kuendelea kujenga ukuta ambao umetugawanya kwa miaka badala ya kutuunganisha''.

Lakini Nieto amesema kuwa urafiki kati ya Mexico na raia wa Marekani utadumu mbali na kutafuta suluhu kuhusu tatizo la wahamiaji.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Mexico Luis Videgaray ambaye yuko mjini Washington amesema kuwa rais huyo bado anaendelea kupima uwezekano wa ziara ya Marekani siku ya Jumanne lakini akaongezea kuwa mkutano huo bado utafanyika kufikia sasa.

BBC

No comments: