ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 16, 2017

Kesi ya Ndama, Mtoto wa Ng’ombe yahairishwa

Kesi inayomkabili mfanyabiashara, Shabani Hussein maarufu Pedeshee Ndama Mtoto wa Ng'ombe imeahirishwa hadi Julai 20, 2017 baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi bado haujakamilika.
Ndama ambaye kwa sasa yupo nje kwa dhamana, kesi yake imetajwa leo(Ijumaa) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.
Ndama kwa sasa anakabiliwa na mashtaka matano baada ya kulikubali shtaka la sita la kutakatisha fedha na kisha kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh 200milioni.
Hatua yake ya kulipa kiasi hicho cha fedha, ilimuepusha na kifungo cha miaka mitano jela.
Ndama yupo huru pia kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambapo kila mdhamini alisaini bondi ya Sh 100 milioni.
Pia mshtakiwa mwenyewe aliweka hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Dola 270,200 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh 600milioni.

No comments: