Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu.
Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo - hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa.
Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya 'wakimbizi wa mazingira' sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. Na hili hii inategemewa kundelea kuongezeka. Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka 2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na Ulaya.
Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa jangwa na kuhama kwa watu. Watu wanaokaa vijijini amabao hutegemea ufugaji wa wanyama,
kilimo na maliasili watakuwa katika hatari zaidi ya kuwa wahanga wa athari hizo, ambazo hujumuisha umaskini, kudorora kwa elimu, ukosefu wa uwekezaji, umbali kutoka huduma muhimu, na kutengwa.
Ni lazima tukabiliane na hali hii na hii inamaanisha kufanya kazi katika ngazi mbili:
Kwanza, ni lazima tusimamie ardhi kwa usahihi,hii ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa jangwa na katika kulinda kiwango chake cha uzalishaji. Hifadhi ya Bayongahewa ya Las Bardenas Reales ya UNESCO iliyoko nchini Hispania inaonyesha kwamba usimamizi wa ardhi kame unaotumia taarifa sahihi, kwa kuzingatia kupishana kati ya matumizi ya malisho, ukulima na vipindi ya bila ya kuilima ardhi hupelekea si tu kusitisha kuwepo hali ya kuenea kwa jangwa lakini pia huleta uwezekano wa kurejesha ardhi kama ilivyokua awali. Hii ndio sababu Programu ya Kimataifa ya UNESCO ya Nishati-Maji imejikita katika kujenga uwezo na kutoa mwongozo wa sera na zana za kushughulikia ukame, kuenea kw jangwa na changamoto zinazotikana na hayo, hasa kuhusiana na usimamizi wa rasilimali maji, kwa njia ya Mtandao wa Kimataifa unaohusika na Maji na Maendeleo ya Taarifa ya Ardhi Kame (G- WADI).
Pili, inatupasa kuimarisha ustahimilivu wa watu walio katika mazingira hatarishi kwa kuwawezesha kuwa na njia mbadala za kujipatia kipato ili tuweze kuuharibu mduara wa kuenea kwa jangwa na madhara yake ya kijamii na kiuchumi ambayo mara nyingi husababisha watu kuyahama makazi yao. Katika kutafuta na kuendeleza elimu na kujenga uwezo katika sayansi, teknolojia na uhandisi, kwa wasichana na wavulana katika nchi zilizo katika hatari zaidi, Programu ya Sayansi ya Msingi ya Kimataifa ya UNESCO inafanya kazi ya kujenga fursa mpya za ajira kwa vijana, kupunguza utegemezi wa rasilimali zinazotegema hali ya hewa, ili kuwapatia watu maisha yenye ustahimivu katika makazi yao.
Katika siku hii, ni lazima tutambue kuwa hali ya kuenea kwa jangwa ni jambo la kimataifa ambalo linalomtishia kila mtu na ni lazima lishughulikiwe kwa pamoja ili kujenga mustakabali endelevu na imara kwa wote.
Ujumbe kutoka kwa Bi. Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, 17 Juni 2017
No comments:
Post a Comment